Wednesday, September 19, 2012

(picha) Mkutano wa Mbunge Msigwa leo soko kuu iringa

Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na wakazi wa iringa mjini umafanyika leo na mbunge wa iringa mjini Mh. Msigwa katika eneo la soko kuu mjini irirnga mbapo wananchi walijitokeza kwa wingi, katika mkutano huu mkubwa Mh. Msigwa ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo swala zito la mauwaji ya mwandishi Daudi mwangosi ambapo Mh. Msigwa amekiri kuguswa sana na kifo cha Mwangosi na hivyo kutangaza maandamano ya amani yatafanyika ilikumuondoa RPC wa iringa michael kamuhanda. 

Katika hatua nyingine Mh. Msigwa aliongoza wananchi wa manispaa ya iringa kuweza kuchangia chochote walicho nacho ilikuweza kuwasilisha pamoja na rambi rambi ambazo zilitumwa awali na wanachadema waliopo uingereza kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania. pia yeye aliongeza laki tano katika fedha hizo, nahivyo kuweaz kupata jumla ya milioni moja na laki nane na sitini na nne (1,864,000) pamoja na mchango wa wananchi ambao waliweza kuchangia papo hapo zaidi ya shilingi laki tatu.

rambi rambi hizo ambazo atakazibidhi mapema kesho kwa familia ya marehemu mwangosi, ambapo ni mjane alie na watoto wa nne.

Msigwa pia aliweza kupata fulsa yakuulizwa maswali na wanachi nakuyajibu, katika mkutano huu Mh. Msigwa na wananchi walikubaliana kuandamana kupinga kuendelea kuwepo kwa RPC Kamuhanda mamanda mano yaamani yanayo tarajiwa kufanyika ijumaa.

No comments:

Post a Comment