Friday, November 1, 2013

Mchango aw Mh. Msigwa tar 31/10/2013

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amesema kitendo cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutengua maamuzi yaliyopitishwa na mawaziri; Dk. John Magufuli (Ujenzi) na Balozi Khamisi Kagasheki (Maliasili na Utalii), wakati ni wa serikali moja ni uthibitisho kwamba utawala wao umefitinika, hivyo hauwezi kuwa na mipango mizuri ya kuliletea taifa maendeleo.

Msigwa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii, alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa hoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015 uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, bungeni juzi. 

Alisema katika moja ya mikutano, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aliwahi kusema kwamba Waafrika wana kila kitu na kwamba hawana sababu yoyote ya kuwa nyuma katika maendeleo isipokuwa tatizo walilonalo ni uongozi.

 Msigwa alisema kinachojadiliwa na wabunge, kuanzia juzi ni mpango wa maendeleo, ambao serikali ndiyo inayousimamia, lakini inashangaza kuona mawaziri wengi hawapo bungeni.

“Angalia mawaziri wako wapi? Spika jana amezungumza hapa. Hawapo. Ambao mnatakiwa mchukue mawazo yetu ili mkaya-accommodate (mkayaingize) kwenye huu mpango. Hampo. Hatuelewi wako wapi. Wapo wawili watatu. Hamtoshi. Hii inaonyesha kwamba hampo serious (makini),” alisema Msigwa na kuongeza:

MAAMUZI YA MIGONGANO, HASARA
“Na ndiyo maana serikali hii hii leo anaondoka Magufuli anasema wenye malori wasimamishe (malori) barabarani. Analeta hasara kwenye Taifa karibu Sh. bilioni 20. Anakuja Waziri Mkuu anasimamisha (amri ya Magufuli). The same government (Serikali ileile).”

Aliendelea kusema kuwa: “Anaondoka Waziri wa Maliasili anasema Loliondo waondoke, anakuja Waziri Mkuu anasimamisha. The same government (serikali hiyo hiyo). Utawala wenu umefitinika. Hatuwezi tukawa na mipango mizuri wakati nyumba yenu haimjaiweka vizuri.”

Waziri Magufuli aliagiza kuondolewa kwa msamaha wa asilimia tano kwa uzito wa magari yanaopita kiwango kiliochopo, msamaha ambao umekuwa ukitumika nchini kwa zaidi kwa zaidi ya miaka saba sasa. Badala yake aliagiza kuanzia Oktoba mwaka huu kila gari litakalozidisha uzioto litatozwa faini ya mzigo uliozidi bila kujali msamaha huo.

Kutokana na maamuzi ya Magufuli ambayo yalianza kutekelezwa Oktoba mwaka huu, wenye malori na mabasi walianza mgomo ambao uliendelea kwa siku kadhaa hasa malori.

Hali hiyo ilitishia kuanguka kwa sekta ya usafirishaji nchini, hivyo kumfanya Pinda kuingilia kati baada ya siku tano kwa kutengua agizo la Waziri Magufuli na kuagiza kurudiwa kwa utaratibu wa zamani wa msamaha wa asilimia tano ya ziada ua uzito ambao hautatozwa faini.

Aidha, Pinda alitengua tangazo la Waziri Kagasheki la kuligawa eneo la Pori Tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro, mkoa wa Arusha.
Katika uamuzi wa Kagasheki alikuwa ametenga kilomita za mraba 1,500 za pori hilo lenye  ukubwa wa kilometa za mraba 4,000 kwa ajili ya kuendelea kuwa chini ya miliki ya serikali na kuachia vijiji kilomita za mraba 2,500.

Tangazo hilo lilitolewa na Waziri Kagasheki, Machi 19, mwaka huu ili serikali ihifadhi eneo la kilomita za mraba 1,500 ambalo alieleza kuwa ni mapito na mazalia ya wanyamapori, pia kutunza ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Tangazo hilo liliibua mgogoro mkubwa.

MAWAZIRI KIDUCHU 
Mbali na Msigwa, wabunge wengine waliohoji sababu za kuwapo mawaziri wachache bungeni wakati wa mjadala huo jana, kinyume cha agizo la Spika wa Bunge, Anne Makinda, ni James Mbatia (Kuteuliwa-NCCR-Mageuzi), Modestus Kilufi (Mbarali-CCM), Kombo Khamis Kombo (Mgogoni-CUF) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini-CCM).

Hali hiyo ilimfanya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, kusimama na kusema kuwapo au kutokuwapo kwa mawaziri bungeni bado wanathamini yanayojadiliwa na wabunge.

Alisema macho na masikio ya serikali wakati wa Bunge yanakuwa Dodoma na kwamba, katika kila ofisi ya serikali kuna runinga, hivyo wanafuatilia yanayojiri bungeni.
Alisema bungeni kuna maofisa wa serikali wanaorekodi kila kinachozungumzwa na kwamba, mawaziri wanapokuwa hawapo bungeni, basi kunakuwa na sababu.

Juzi wakati akiahirisha Bunge, Spika Makinda aliwataka mawaziri wote kwenda bungeni jana kwa ajili ya majibu kwa kuwa hoja (Mpango wa Maendeleo wa Taifa) inayojadiliwa inagusa wizara zote.

Awali, Msigwa alisema katika siku za hivi karibuni lugha ya viongozi imekuwa ni kusisitiza kuomba amani na utulivu kila mahali wanaposimama.
 Lakini akasema amani ni tunda la haki, ambayo ikiwekwa mahali pake watu hawahitaji kugombana na pia hakuwezi kutokea fujo.

“Amani ya nchi hii haitalindwa na vifaru vingi, haitalindwa kwa kuongeza wanajeshi wengi. Amani ya nchi hii itatokana pale haki, wananchi wanapopata haki zao, wananchi wanapotendewa haki, wananchi wanapopata huduma zile ambazo wanastahili kuzipata,” alisema Msigwa.

Alisema kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa katika mfumo wa chama kimoja, lakini pamoja kuwako kwa mabadiliko ya mfumo huyo kwa kuanzishwa vyama vingi nchini, kuna watu kwenye fikra zao hawaamini hilo.

 “Kwa hiyo, wanaona watu wengine ambao hawana imani kama yao, ni watu wanaoleta vurugu,” alisema Msigwa na kuongeza:

“Nilitaka niwakumbushe walioko madarakani kwamba we are here to stay (tutaendelea kuwako). Tuko hapa kwa mujibu wa katiba, sisi siyo intruders (wavamizi), ni Watanzania, watawala mnatakiwa mu-accommodate (kuchukua) mawazo tunayoyaleta hapa kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu. Aidha, tuishi pamoja kama Watanzania na kujenga Taifa letu.”

Alielezea hali ya kuzorota kwa maendeleo kwamba kwenye majimbo mpaka leo hata nusu ya fedha iliyotolewa mwaka jana haipo, serikali inathubutu kuja na mpango mpya, ambao hauna jipya.

Msigwa alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ni ya pili baada ya Wizara ya Nishati na Madini kuiingizia serikali fedha za kigeni, lakini katika mpango huo imewekwa kama Chuo cha Mkwawa, ambacho kimeelezewa kwa uchache.

Alisema Mpango huo hauonyeshi mazingira ya kuiwekea maliasili ili kuongeza utalii nchini, kama yale ambayo serikali imewawekea wawekezaji wa madini, ambao wameondoka na kuwaachia Watanzania mashimo.

MWAIPOSA: VIPAUMBELE VICHACHE
Mbunge wa Ukonga (CCM), Eugen Mwaiposa, aliishauri serikali kuangalia vipaumbele vichache ili iwe rahisi kuvitekeleza.

MSHAMA: RAIS ANADANGANYWA

 Mbunge wa Nkenge (CCM), Assumpter Mshama, alisema kuna watu, ambao hawamwambii Rais ukweli hali ambayo imekuwa ikikwamisha mambo.
“Hivi kweli inafikia tarehe 30 wabunge hatujalipwa mishahara kama unafanya kazi kwa mhindi?” alihoji Mshama.

NTUKAMAZIMA: AIBU YA TANZANIA

Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratias Ntukamazina, alisema ni aibu kwa nchi kama Rwanda kuwa na ndege saba, lakini Tanzania isiwe na ndege hata moja.

MBATIA:  UMASIKINI WA MIPANGO

Mbatia alisema tatizo kubwa la serikali ni umaskini wa mipango inayopanga na kushauri iwekeze kwa kiasi kikubwa kwenye bandari ili kuepuka mazoea ya kukopa.
CHANZO: NIPASHE

Sunday, September 29, 2013

Hotuba ya Mh. Msigwa

HOTUBA YA UFUNGUZI WA MJADALA WA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI KAMA ULIVYOANDALIWA NA MANET (Mazingira Network Tanzania) MR HOTEL, IRINGA.
Ndugu wageni waalikwa, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa kunipa nafasi ya kushirikiana nanyi leo hii hapa kama mmoja wa wadau muhimu katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori.
Kwa muda mrefu nimekua mstari wa mbele katika vita dhidi biashara haramu ya wanyamapori si kwa kua nina maslahi binafsi na sekta hii, bali kwa kuwa nina dhamana hiyo kama mtanzania yeyote yule na kwa kuwa ni moja ya wajibu wa kila mtanzania kama ambavyo katiba ya nchi yetu inavyotuongoza. Ibara ya 27(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kwamba “Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine”, Pia katika ibara hiyohiyo ya 27 (2) inasema kwamba “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao”, Ni dhahiri matakwa haya ya kikatiba hayatenganishi utu wa mtu kwa mujibu wa kikatiba ndani ya nchi katika nafasi zake kimamlaka katika usimamizi wa rasilimali za taifa.
Ndugu wageni waalikwa,napenda kutambua mchango wa MANET pia kama wadau muhimu hasa katika kuhakikisha kuwa mazingira ya taifa letu hususani katika sekta za misitu, uvuvi na wanyamapori vinalindwa si tu kwa matumizi ya leo bali kwa ajili ya vizazi vijavyo. Zaidi natambua mchango wa MANET kama shirika ambalo lipo mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa jamii inakua mstari wa mbele kupiga vita rushwa hasa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mamlaka za serikali za mitaa.
Ni jambo la kujivunia kuwa mzawa wa nchi ambayo imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi huku tukiwa tumejaliwa maliasili na vivutio vya kutosha Duniani. Lakini ni jambo pia la kusikitisha, kuona kuwa tupo katika taifa ambalo sasa lipo katika ramani ya dunia kwa kushindwa kusimamia, kudhibiti na hata kutunza rasilimali hizo hasa wanyamapori ambao ndio moja ya utambulisho wa Taifa letu duniani. Takwimu mbalimbali zimeendelea kuishtua dunia juu ya kasi ya vitendo hivi vya biashara haramu hasa kwa nchi ambayo watu wake wanasifika kwa ukarimu na amani.
Ndugu wageni waalikwa, suala la biashara haramu ya wanyamapori nchini limeendelea kukua kwa kasi ya ajabu huku Serikali ikionesha wazi kushindwa kudhibiti suala hili na hivyo kutoa mwanya kwa majangili kuendelea kuteketeza wanyamapori huku baadhi ya viumbe hai vikiwa hatarini kutoweka kabisa katika ramani ya Taifa letu.
Watanzania wenzangu, ni masikitiko makubwa kuona kuwa mkutano mkuu wa wanachama wa Mkataba wa Biashara wa Viumbe walio hatarini (The Convention on Trade in Endangered Species - CITES) uliofanyika Bangkok, mwaka huu Tanzania na Kenya zilitajwa kati ya nchi nane duniani, ambazo zinaongoza kwa biashara haramu ya wanyamapori na hivyo mkutano ule ulipendekeza kuwa nchi hizi lazima ziwekewe vikwazo vya biashara.
Swali la msingi la kujiuliza , ni kwa nini kama Taifa tufikie mahali ambapo tunaweza kuwekewa vikwazo vya biashara kwa kushindwa kutekeleza wajibu wetu na kulinda maslahi ya watu wachache? Ukiangalia takwimu mbalimbali nchini na za kimataifa, Taifa letu limeendelea kuwa katika ramani ya dunia kwa kuwa moja ya nchi vinara zinazotia doa hasa kwa biashara haramu ya wanyamapori, hali inayohatarisha maisha ya baadhi ya viumbe hai.
Mara kadhaa tumesikia viongozi wa Serikali wenye dhamana wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza. Mara kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu. Serikali imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Jambo moja la msingi ambalo ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko lake maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema yafuatayo
“Uhai wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi,sio muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye”.
Mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa wakati huo tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa Serikali wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za baba wa taifa letu ,vinatimizwa.
Kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya kuwawakilisha, nawiwa kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau nambari moja wa kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa inalitia hasara taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya wanyamapori kwa vizazi vijavyo.
Nachukua nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria.
Ndugu wageni waalikwa, pamoja na kuisisitiza Serikali kutimiza wajibu wake wa kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori ni lazima pia mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kuongeza juhudi zao kuhakikisha kuwa elimu kwa umma inatolewa ili kuongeza nguvu ya pamoja katika masuala ya kulinda wanyamapori.
Binafsi, napenda kuchukua nafasi hii kuupongeza uongozi wa MANET kwa kuwa mdau muhimu katika kuhamasisha umma na jamii ya kitanzania katika utunzaji wa mazingira na pia katika kutoa mchango wake mkubwa dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori hasa kwa kupitia fursa mbalimbali kama hizi.
Nawashukuru sana MANET kwa kutambua mchango wangu katika suala hili na kwa kunipa fursa ya kuzungumza machache juu ya "Biashara haramu ya wanyamapori".
Napenda pia kuwapongeza MANET kwa kuandaa mjadala huu wa Vita dhidi ya biashara ya wanyamapori ambao umewashirikisha wadau mbalimbali. Katika majadiliano mbalimbali yatakayofanyika leo, ningependa kuona mjadala huu si tu utatoa changamoto bali pia utatupa njia mbadala na bora za kuweza kukabiliana na biashara ya wanyamapori ikiwemo kutoa maazimo ya nini kifanyike ili kutatua suala hili pale mjadala utakapokamilika.
Napenda tena kuchukua nafasi hii, kuwashukuru kwa heshima mliyonipa kama mgeni rasmi, na nawatakia majadiliano mema yatakayoleta majibu sahihi.
Kwa idhini mliyonipa natangaza rasmi kuwa, mjadala huu sasa umefunguliwa.
Kwa pamoja, tunaweza.
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni sana.

.......................................................
Mch. Peter Simon Msigwa,(MB)
Waziri kivuli wa Maliasili na Utalii
Iringa Mjini
28.09.2013

Friday, September 27, 2013

Video Mbinu chafu za uongozi wa ccm iringa dhidi ya Chadema/Msigwa.Hii inakuja baada ya Mh.msigwa kufanya mkutano wa hadhara mjini Iringa akiwataka wananchi
1. Waache maramoja kuchangia shughuli za mwenge kwa I budget ya mwenge imeshapitishwa bungeni, pia fedha inayo Changishwa haina ukaguzi wowote wa CAG kuonyesha imetumika vipi, alisema hizo pesa badala yakuzipoteza kwenye shughuli za mwenge ni bola wakalipia kodi ili kuongeza Maputo.
2.Na pia katika mkutano huu aliagiza nguvu ya umma kutumika(kuyapiga mawe) magari ya manispaa ya iringa iwapo yataendelea Kuwa miss used na kipindi viongozi wa ccm (kinana na mwenzake nape) wanapokuja jimboni Iringa.

Saturday, September 14, 2013

kutoka libraly ya picha


kampeni za 2005 nikiwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjn kupitia TLP na lyatonga mrema.


nilipo kuamjasilia mali kwa kuuza mitumba na umachinga way back


my wedding day


graduation day


siku ya mahafali nilipo maliza degree 

Wednesday, September 4, 2013

Safari ya Mwanza, katika mazishi ya Mch. Moses kulola.


safarini njiani kuelekea mwanza nikiwa na mbunge wenje


katika ibada ya kumuaga Mch. Moses kulolatulikutana na masanja, hapa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.

Monday, September 2, 2013

kutoka ukuta wa facebook ya Mh. Msigwa

Nani mwongo Kati ya Mimi na Kagasheki. Haya ndio maadili ya UONGOZI..?haiwezi kiongozi Waziri msimamizi wa ngorongoro, mke wake apewe pesa kwa ajili ya foundation ya familia Yao. Eti Waziri anasema namfuata! Ninachotaka Waziri ajibu hoja .akisema Mimi natumiwa na mafisadi bado hujajibu hoja yangu akatae hapa Kama hajavunja utaratibu na kukiuka maadili ya UONGOZI